
Ripoti ya Tume Huru ya kuchunguza vurugu za wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania 2025 imependekeza kutengwa siku maalum ya kuwakumbuka waliofariki kutokana na vurugu za Oktoba 29.
Akisoma mapendekezo yaliyotolewa na tume hiyo kwenye ripoti iliyotolewa leo, Mwenyekiti-Jaji Mstaafu Mohamed Othman Chande ameshauri pia kuendeleza kazi ya tume hiyo ili ifanye uchunguzi mahsusi kuhusu vurugu hizo.
Mengine yaliyopendekezwa na tume ni pamoja na kufanyia kazi na kurekebisha uhalali wa matumizi ya silaha za moto ufanyiwe kazi kuzingatia mazingira yaliyokuwa kwenye tukio hilo kwa wakati na muda huo.
“Maridhiano na muafaka ni hatua muhimu katika kuponya majeraha katika kuleta Amani. Maridhiano yawe mtambuka kisiasa, kijamii na kiuchumi” amesema Jaji Chande
Mengine ni kuundwa kwa katiba mpya, kuwepo kwa majadiliano baina ya viongozi wa dini na kukubaliana kuwepo kwa mipaka kati ya dinia na siasa, na kuundwa Baraza la wazee lisilo rasmi litakalosaidia ushirikiano na maridhiano.
