

Praise Wisdom kutoka Kampala, Uganda ameibuka mshindi wa mashindano ya Bongo Star Search (BSS) msimu wa 16.
Fainali ya mashindano hayo ya kihistoria imefanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa HaddyPro, Mbezi Beach Julai 11, 2026.
Mshindi huyo amejinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 taslimu pamoja na gari mpya.
Msanii mwenye jina So Fire kutoka mkoani Mbeya Tanzania, ameshika nafasi ya pili na kuondoka na jumla ya Shilingi Milioni 10 (Milioni 5 kutoka kwa wadhamini wakuu CRDB Bank na Milioni 5 zingine kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila).
