
Mgawanyiko wa kimitazamo ndani ya chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, umechukua sura mpya kufuatia majibizano makali ya mtandaoni kati ya mwanaharakati mashuhuri Mange Kimambi na Mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Godbless Lema.
Majibizano hayo yanaakisi joto la kisiasa lililopo ndani ya chama hicho huku kukiwa na madai ya kuwepo kwa “maridhiano ya siri” na chama tawala (CCM).
Tuhuma za ‘Kununuliwa’ na Siasa za Makundi
Mjadala huo uliibuka baada ya Mange Kimambi kuweka bandiko mtandaoni akidai kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA “wamefika bei” na kukubali maridhiano na CCM.
Kimambi alidai kuwa vita ya kisiasa inayomkabili Mbunge wa zamani wa Tarime Vijijini, John Heche, inasukumwa na viongozi hao ili kumg’oa na kuweka mtu atakayekuwa tayari kushirikiana na serikali.
”Heche anapigwa vita sababu kuna viongozi ndani ya CHADEMA wamefika bei ya maridhiano na CCM, so wanajaribu kumuondoa Heche ili waweke mtu ambae atafanya maridhiano,” alidai Kimambi akiongeza kuwa Heche na Tundu Lissu wanahitaji uungwaji mkono wa dhati kwa sasa.
Akijibu mapigo hayo kwa utulivu, Godbless Lema alimtaka Kimambi kuwa na subira na kufanya uchunguzi kabla ya kutoa hitimisho linaloweza kukiumiza chama. Lema alieleza kusikitishwa kwake na tuhuma hizo lakini akasisitiza kuwa hatatenda jambo lolote kwa kufuata “ego” yake, bali atalinda heshima ya CHADEMA.
Lema alidokeza kuwa maamuzi rasmi ya Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi mkoani Kigoma yanatarajiwa kutangazwa hivi karibuni, na ndiyo yatakayotoa mwelekeo.
“Kwa sasa sitajibu chochote kwa heshima na hadhi ya chama chetu, nikiamini kwamba maazimio ya Kamati Kuu yaliyofanyika Kigoma yatasomwa hivi karibuni… Nitaendelea kuitanguliza taasisi yetu mbele kuliko ego yangu,” alisema Lema.
Licha ya ombi la Lema, Mange Kimambi alikuja juu upya akitaka majibu ya maswali magumu yanayowatatiza wananchi. Katika hoja zake, Kimambi alimtaka Lema kufafanua sababu zilizomfanya Lema na Joseph Mbilinyi (Sugu) kufanya mkutano tofauti siku ambayo aliyekuwa mwanachama wao, Peter Msigwa, alikuwa akipokelewa (baada ya kuhamia CCM), hatua inayotafsiriwa kama ukosefu wa umoja.
Pia amemtaka sababu za Lema kutohudhuria au kutoa kauli yoyote kuhusu msiba wa aliyekuwa dereva wa John Heche.
Kuhusu kimya cha Viongozi, Mange amehoji sababu za Lema kukaa kimya wakati Makamu Mwenyekiti (Tundu Lissu) akishambuliwa kwa tuhuma mbalimbali bila kumtetea.
Hata hivyo, Lema ameshikilia msimamo wake wa kutozungumzia masuala ya ndani ya chama kabla ya Kamati Kuu kutoa tamko rasmi, huku akitoa kauli ya fumbo iliyoacha maswali mengi:
“Kamati Kuu itasema, nikisema sasa nitakuwa nakosea. Jambo moja la msingi ni hili, nitasema ikiwa ni lazima na nitasema bila hofu… Dada, niombee nisiongee
