WINO Ripota
Zimebaki siku 16 kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27 lakini leo Chama Kikuu cha Upinzani hapa nchini Chadema kimeibua wimbi jipya wakidai wagombea wa chama hicho ambao awali walichaguliwa kuwania nafasi za uongozi wa serikali za mitaa, wameenguliwa.
Akizungumza na Wino Tanzania, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema, ukiachilia mbali kufungwa kwa ofisi za wasimamizi wa uchaguzi na zile za vitongozi na vijiji, ambako wagombea walitakiwa kuweka pingamizi zilikuwa zimefungwa.
“tarehe 10 ilikuwa siku ya kuwasilisha mapingamizi lakini ofisi nyingi za watendaji, wa kata na vijiji, ofisi ambazo zilikuwa zimefungwa ni nyingi, wilaya ya Kinondoni dar es salaam zilikuwa zimefungwa, kule kibamba, zilikuwa zimefungwa, “ amesema Mrema
Amesema licha ya ofisi hizo kufungwa na kuzuia wagombea kuwasilisha mapingamizi lakini wimbi CHADEMA kimebaini kuwa baadhi ya walioteuliwa awali, majina yao yamekatwa.
“Wagombea ambao Novemba 8 majina yao yalipitishwa kugombea uongozi wa serikali za mitaa, jana Novemba 10, tumebaini yameenguliwa, ikidaiwa kuwa yaliwekewa mapingamizi,” amesema Mrema
Hata hivyo, Tamisemi, kupitia Katibu Mkuu, Adolph Ndunguru imesema, vyama vingine viliweka mapingamizi wakati tayari zoezi limeshafungwa.
“Lakini bado wanaweza kuendelea na kukataa rufaa kwa mujibu wa kanuni,” amesema
Kadhalika Ndunguru amesisitiza kuwa vyama vinavyodai ofisi zimefungwa vilete Ushahidi ili TAMISEMI ishughulikie.
Mwanachama wa Chadema, aliyechukua fomu kuwania uongozi wa serikali za mitaa, Fredinard Ruge amesema, Novemna 9 na 10, watendaji hawakufungua ofisi na hali hiyo ilisababisha washindwe kuweka pingamizi.
