Leo maelfu ya wanafunzi wa kidato cha nne hapa nchini wanafanya mitihani yao ya kumaliza elimu ya sekondari.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Dorothy Gwajima, amewaandikia akisema:
“Kwenu watahiniwa wa mtihani wa kumaliza kidato cha nne, unaoanza tarehe 11 Novemba, 2024: nawatakia kila la heri na ufaulu mwema.
Naamini maandalizi yenu, ujasiri wenu na utulivu wenu ndiyo nguzo ya mafanikio yenu ya kufaulu mtihani huu muhimu katika hatua ya kuitafuta elimu.”
Na sisi WINO Tanzania, tunaungana na Watanzania wengine tukiwatakia wanafunzi wa kidato cha nne, utulivu na mafanikio katika mitihani yao leo.

