Wino Ripota
Tanzania, Kenya na Afrika Kusini zimetajwa kushikilia uti wa mgongo wa utalii barani Afrika kwa asilimia 64.
Kwa mujibu wa ripoti mpya ya Hali ya Safari za Kitalii Duniani, 2026, iliyoandaliwa na taasisi ya utalii ya Go2Africa ikihirikiana Chama cha Safari na Utalii Africa (ATTA) nchi hizo tatu ndizo zinazopokea idadi kubwa ya watalii ukilinganisha na nchi nyingine.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, yapo mataifa ya Afrika ambayo yameongeza idadi ya watalii kwa mwaka 2025 kama vile Botswana,Malawi na Madagascar.
Kadhalika ripoti hiyo, imebaini kuwa asilimia 85 ya wasafiri wanaokuja Afrika huwa wana taarifa kamili ya kule wanakokwenda na kati yao asilimia 35 hufahamu miaka miwili kabla ya safari. Hata hivyo ripoti hiyo imeonyesha kuwa Kenya imeipiku Tanzania katika nchi zinazotembelewa zaidi wakati Madagascar ikipanda ngazi zaidi katika kutembelewa na watalii
