Mraghibishi wa mitandao ya kijamii, Ashelee Robinson maarufu kama Ashelee Jenae, raia wa Marekani, Miami, amekutwa akiwa amefariki dunia hotelini kwake visiwani Zanzibar ambako alikuwa katika mapumziko.
Jenae, alifika Tanzania akiwa na mchumba wake, Joe McCann, kwa ajili ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kuvishwa pete ya uchumba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Benedict Mapujira ameiambia Wino kuwa wamethibitisha kuwa Jenae alifariki kwa kujinyonga wa kutumia kipande cha nguo, chumbani mwa hoteli.
Hata hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, imebainika kuwa, Jenae alikutwa amefariki katika chumba cha hoteli aliyofikia, visiwani Zanzibar, Serval Wildlife Resort, huko visiwani Zanzibar.
Jenae alituma chapisho lake la mwisho Aprili 5, siku ya kuzaliwa kwake akisema: “Ukurasa wa 31, nipo katika sehemu sahihi kabisa”

Hata hivyo marafiki wa Jenae, wameandika kupitia machapisho yake ya mwisho, wakisema, haiwezekani Jenae kujiua na wakata ukweli utafutwe kuhusu kifo chake. Mpaka sasa Joe McCann mchumba wa Jenae haulikani alipo, ingawa mamlaka hazijamshutumu kwa lolote kuhusiana na kifo cha mchumba wake.
