Wino Tanzania, Ripota
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi baada ya kifo cha Mfanyabiashara kijana, tajiri raia wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo na kumtaja kuwa mwenye maono na aliyegusa maisha ya wengi.
“Ni kwa masikitiko makubwa ninapoomboleza kifo cha mfanyabiashara wa Zimbabwe, Bw. Wicknell Chivayo, mke wake mpendwa, pamoja na watu wengine watatu, ambao kwa huzuni kubwa wamepoteza maisha katika ajali ya helikopta iliyotokea Marondera”
“Zimbabwe na Afrika zimepoteza kijana mjasiriamali mwenye maono, aliyegusa maisha ya watu wengi”
“Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatoa pole zangu za dhati na za kutoka moyoni kwa Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe; familia ya Chivayo; familia za wote waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo; pamoja na wananchi wa Zimbabwe” amesema Rais kupitia akaunti yake ya X.
