- Afya ya Uzazi kwa vijana yazungumzwa, wadau wakitaka kuboreshwa kwa sera

Kampala.
Wakati Siku ya kimataifa ya Vijana ikitarajiwa kuadhimishwa Agosti 12, vijana kutoka Afrika wametaja changamoto zinazowakabili, Youth Summit, Kampala.
Zinazojumuisha ukosefu wa ajira, masuala ya usalama na ukabila.
Wakizungumza katika Mkutano wa Vijana wa Afrika wa Fourth B!ll Now Now (BNN) uliofanyika jijini Kampala, vijana walijumuika na kuzibainisha changamoto na fursa walizonazo katika maeneo yao. Huku wadau wengine wakioshiriki wakishauri suluhisho.
Esther Keji kutoka Sudan Kusini, amesema ukosefu wa usalama ni miongoni mwa vikwazo vikubwa vinavyowakabili vijana nchini humo. Alisema kuwa migogoro inaendelea kuvuruga elimu, shughuli za kujipatia kipato na ushiriki wa vijana katika masuala ya kiraia.
“Tunatamani kuwekeza zaidi katika ujenzi wa Amani na fursa jumuishi zitazowezesha vijana kuendelea na maisha na kufikia maendeleo yao” Keji.
Ajenda ya 2063, iliyopitishwa Januari 2015, inawaweka vijana katikati ya ajenda ya maendeleo ya Afrika.
Kwa hili, mfumo huu unalenga kukabiliana na changamoto zinazowakabili vijana barani Afrika.
Hizi ni pamoja na ukosefu wa ajira, upatikanaji mdogo wa elimu bora, na uwakilishi usiotosheleza katika uongozi na maamuzi.

Mshiriki kutoka Uganda, Mukiibi Sharifi, ambaye pia ni mwakilishi wa Programu ya 03 Plus ya UNESCO, alisistiza wawekeze katika ubunifu, uvumbuzi na maendeleo ya ujuzi wa vijana ili kufungua fursani ya uchumi wa ubunifu na uchumi wa kidijitali unaokua barani Afrika.
Kwa mujibu wa Umoja wa Afrika (AU), karibu asilimia 60 ya wakazi wa Afrika wana umri wa chini ya miaka 25, hali inayoifanya Afrika kuwa bara lenye vijana wengi zaidi duniani.
Humphrey Nabimanya, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Reach A Hand Africa, amepongeza Mkutano huo kwa kuwa na mwelekeo wa utekelezaji, tofauti na mikutano mingi inayofanyika bila hatua madhubuti.
“Kuna mijadala na mikutano mingi inayowahusisha vijana ambayo huwa ya kiishara tu, lakini mkutano wa mwaka huu una maana kwa sababu umejikita katika kuchukua hatua,” alisema
Chini ya Dira ya 1 na Dira ya 6, inasisitiza umuhimu wa kuunda ajira. Kuendeleza ujuzi katika sayansi na teknolojia, pamoja na kuwawezesha vijana kutumia ipasavyo fursa zinazotokana na ongezeko la idadi ya watu barani Afrika.
Majadiliano katika Mkutano huo yalijikita katika maeneo sita ya kipaumbele.
Hayo ni Afya ya Uzazi na Ujinsia (SRH).
Pia, ni Afya ya Akili, Ujasiriamali na Biashara, Elimu na Ujuzi.
Vilevile, Mabadiliko ya Tabianchi na Uchumi wa Kijani na Teknolojia yenye Uwajibikaji na Akili Bandia (AI).
