
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche, amekiri kuwa chama hicho kilikuwa na msimamo wa kutoshiriki uchaguzi mkuu wa 2025 hadi pale mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi yangefanyika.
Heche ametoa kauli hiyo leo Septemba 15, wakati akihojiwa na Wakili Katuga katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, ambapo alithibitisha kuwa msimamo wa ‘No Reforms, No Election’ ulikuwa wa chama hicho.
Katika mahojiano hayo, Heche alisema Chadema ilikuwa na haki ya kikatiba kuamua kushiriki au kutoshiriki uchaguzi mkuu, huku akisisitiza kuwa uchaguzi unaostahili kushirikishwa vyama vya siasa ni ule ulio huru na wa haki.
Alipoulizwa kuhusu idadi ya vyama vya siasa vilivyosajiliwa nchini, Heche amesema vilikuwa 19, lakini hakujua misimamo ya vyama vingine kuhusu uchaguzi.
Wakili Katuga pia alimuuliza Heche kuhusu madai kwamba viongozi wa Chadema walikuwa wakipanga kuzuia uchaguzi kwa kukutana na viongozi mbalimbali, akiwamo Jaji Joseph Warioba na Sheikh Ponda.
Heche amekataa kuwa kukutana na Jaji Warioba kulikuwa sehemu ya mipango ya kuzuia uchaguzi, lakini alikubali kuwa Chadema iliwahi kukutana na Sheikh Ponda.
Katika sehemu nyingine ya mahojiano, Heche alikiri kuwa alishawahi kusema uchaguzi wa mwaka 2025 hautafanyika, lakini alipoulizwa kama alikumbuka kauli hiyo alisema hakumbuki.
Pia alikiri kuwa aliwahi kueleza kuwa Chadema iliwatembelea viongozi wa dini, ingawa alisema hakumbuki iwapo ushahidi wa ziara hizo unafanana na ushahidi alioutoa mahakamani.
Wakili Katuga alimuuliza kuhusu mkutano wa Chadema wa Aprili 3, 2025, akitaka kujua kama Lissu aliwahi kusema watazuia au kuvuruga uchaguzi. Heche alithibitisha kuwa alimsikia mwenyekiti huyo akisema watakuzuia uchaguzi na kwamba watavuruga uchaguzi.
Hata hivyo, Heche alisema hakumsikia Lissu akisema “tutahamasisha uasi”. Pia alisema Lissu hakuwapa wao njia za kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi au “kukinumua”.
Heche pia alieleza kuwa katika msimamo wao kuhusu uchaguzi, walikuwa wakilalamikia mapungufu katika mfumo wa uchaguzi na kutaka mabadiliko.
Katika mahojiano hayo, Wakili Katuga aliendelea kumhoji Heche kuhusu ushahidi wake kuhusu matukio ya Oktoba 29 na Tume ya Rais iliyoundwa kuchunguza matukio hayo.
Heche alikiri kuwa Chadema haikukubaliana na muundo wa tume hiyo, lakini alipoulizwa kama chama hicho kilikataa kuipa ushirikiano, alisema: “Sikusema hilo.”
Mahojiano zaidi haya hapa:
Wakili Katuga: Waambie majaji kama ni ushshidi
wako kwamba mshtakiwa alisema hatuko tayari kushiri uchaguzi wa namna hii,
mlipokuwa mkipita kwa wadau?
Heche: Sahihi
Wakili Katuga: Nitakuwa sahihi, nikisema msimamo
umekuwa ni kutoshiriki kwenye uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike?
Heche: Sahihi
Wakili Katuga: Nakumbuka uliiambia Mahakama kwamba
Lissu alipokuwa akipita kwa wadau hakuna sehemu alitumia neno kuhamasisha uasi?
Heche: Ni sahihi.
Wakili Katuga: Kama kutakuwa na shahidi alisema
hata kwa wadau alitumia neno kuhamasisha uasi, ushahidi huo utakuwa wa uongo au
ukweli?
Heche: Inategemeana na context
Wakili Katuga: Hizo shahidi mbili haziko sawa au ziko sawa?
Heche: Ziko sawa.
Wakili Katuga: kwahiyo ni ushshidi wako kwamba
alikuwa anatumia neno tutahamasisha uasi kwa wadau na wewe unasema hajatumia
maneno tutahamasisha uasi, haya maneno yako sawa?
Heche: Nilisema maneno ni hayo hayo lakini
Context ndizo zinatofautiana.
Wakili Katuga: Ulisema vyombo vya habari havitoi
nafasi sawa kwa wagombea?
Heche: Ni sahihi
Wakili katuga: Uliiambia Mahakama mengi kuhusu
mapungufu ya uchaguzi
Heche: Sahihi.
Wakili katuga: Ulieleza ni aina gani ya mfumo wa
uchagizi unazuia vyombo vya habari visitoe nafasi sawa?
Heche: Nilieleza
Wakili katuga: ulieleza ni sheria ipi inayowaambia
waandishi wa habari toeni habari hii na hii msitoe?
Heche: Kuna upendeleo
Wakili Katuga: Umesema kutokana na kutokuwa na
usawa wa sheria za uchaguzi, kwamba kuna sehemu mawakala wamekuwa wakipata
usumbufu wa viapo unakumbuka
Heche: Nilisema
Wakili Katuga: Waambie majaji kama ulitaja vituo
ambavyo mawakala walizuiwa.
Heche: Nilisema Kwa nchi nzima
Wakili Katuga: Unajua au hujui kama uliposhinda
uchaguzi, pia ulituhumiwa kufanya fujo na kuingiza kura feki?
Heche: Hilo Unajua wewe, sijui.
Wakili katuga: Unajua au hujui kwamba mwanasiasa
akishindwa hakubali kiurahisi?
Heche: Chadema ukishindwa unarudi zako
nyumbani.
Wakili Katuga: Waambie majaji kama wewe
ulivyoshindwa ulikubali?
Heche: Uchaguzi haukuwa huru na haki
nilipoteza
Wakili Katuga: Ulisema ulishinda ubunge mwaka gani?
Heche: 2015
Wakili Katuga: Uchaguzi wa 2015 ulikuwa huru na
haki?
Heche: Uchaguzi wa 2015 ulikuwa na figisu.
Wakili Katuga: Uchaguzi wa 2015 uliochaguliwa
Uliukubali au uliukataa?
Heche: Niliukubali kwa vita, japo ulikuwa
na makosa mengi.
Wakili Katuga: Ulikuwa wa uhuru na haki au haukuwa
huru na haki jimboni kwako wewe?
Heche: Haukuwa huru na haki
Wakili Katuga: Waambie majaji kama wewe ni mtu wa
haki kama unavyojiita, wambie majaji ulikuwa na uwezo wa kuukataa ushindi wako
au ulikuwa huna?
Heche: (Heche akawa mbishi majaji
wakamueleleza kwamba anaulizwa yeye kwa nafasi yake.)
Wakili Katuga: (wakili katuga akarudia swali)
Heche: Nilikuwa sina uhuru.
Wakili Katuga: kwa hiyo ulilazimishwa kukubali
matokeo?
Heche:
Wakili Katuga: Waambie majaji, ni sheria ipi
inayokulazimisha kwamba ukitangazwa mshindi huna uwezo wa kukataa?
Heche: wananchi, Waheshimiwa majaji siyo
sheria. Siijui.
Wakili katuga: Wewe ukitangazwa kuwa mshindi, huo
uchaguzi hauwi batili?
Heche: Sio
kweli.
Wakili Katuga: Ni kweli au siyo kweli uliingia
bungeni kwa uchaguzi uliokuwa batili?
John Heche: Ni sahihi.
Wakili Katuga: Waambie majaji kama ni kosa au siyo
kosa kama huyu mkurugenzi uliyesema alistaafu ukurugenzi wa tume ya uchaguzi
akaenda kugombea kupitia Ccm, je angekuja chadema ingekuwa kosa au siyo kosa?
Heche: Mtu yoyote
aliyekuwa mtumishi wa umma, nitakuwa sahihi ninkisema anahaki ya kujiunga na
chama cha chadema?
Heche: Ni sahihi
Wakili: The same pia, mtu yoyote aliyemaliza
utumishi wake, anaweza kujiunga na chama kingine chochote?
Heche: Hayo ni maneno yako
Wakili Katuga: Umetaja sheria yoyote inayomkataza
mtumishi wa umma kutojiunga na ccm baada ya kustaafu?
Heche: Sijataja.
Wakili Katuga: ulisema chadema mlikuwa tayari
uchaguzi usogezwe mbele
Heche: sahihi
Wakili Katuga: ulisema ni sheria gani inayoruhusu
uchaguzi usogezwe mbele ili kupisha mabadiliko?
Heche: sikueleza
Wakili katuga: ulisema mlienda Nairobi kumuona
Raila odinga, Waambie majaji kama kule pia mlimuambia Raila Odinga mnaenda
kuzuia uchaguzi, mnaenda kukinukisha, mnaenda kuzuia uchaguzi, waambie
waheshimiwa Majaji.
Heche: Tulimwambia matatizo ya uchaguzi. Waheshimiwa majaji mambo tuliyoyazungumza ni
yaleyale.
Wakili Katuga: Taarifa zinazotolewa na Brenda Rupia zinakuwa ni maelekezo ya chama au
utashi wake binafsi?
Heche: Katibu mkuu na ofisi yake ndiyo inamuelekeza kutoa taarifa.
Wakili Katuga: Mpaka unakuja kutoa ushahidi hapa, ulifanikiwa kusoma mashtaka au
hukosoma?
Heche: Nilisoma
Wakili Katuga: waambie waheshimiwa Majaji kama kuna sehemu yoyote mshtakiwa
anashtakiwa kwa kuandaa mkutano?
Heche: Sijui
Wakilli Katuga: Ulisema tuhuma za mshtakiwa za kuwaalika waandishi wa habari siyo za
kweli
Heche: sahihi
Wakili Katuga: kuna sehemu mshtakiwa anashtakiwa kwa kuwaalika waandishi wa habari?
Heche:
Wakili Katuga: waambie majaji kama mwenyekiti alitaka au hakutaka hotuba yake iwafike
Umma?
Heche: Siwezi kukumbuka
Wakili Katuga: ni kweli au siyo kweli kwamba tarehe 3, April 2025 katika mkutano
uliofanyika ndani huku waandishinwa habari wakiwepo?
Heche: Sikumbuki
Wakili Katuga: Mwenyekiti alikuwa na uwezo au hakua na huo uwezo wa kuwaondoa au
kutoongea mbele ya waandishi wa habari?
Heche: mkutano uliandaliwa na sekretarieti. Kwahiyo sijui
Wakili Katuga: ulimuona au limshuhudia akilazimishwa kuongea mbele ya waandishi wa
habari?
Heche: Nimesema Sijui
Wakili Katuga: waambie majaji, mbali na mwaliko, kama unafahamu au hifahamu kulikuwa
na hotuba rasmi aliyoandaliwa mwenyekiti.
Heche: Sifahamu
Wakili Katuga: mikutano ya chadema huwa inahifadhi kumbukumbu?
Heche: Siyo yote.
Wakili Katuga: Nani alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa tarehe 3, aprili 2025?
Heche: Haukuwa na mwenyekiti.
Wakili Katuga: Naninalikuwa mzungumzaji mkuu?
Heche: Mwenyekiti wa Chama Taifa
Wakili Katuga: Waambie majaji wewe kama wewe ukiongea kwenye huo mkutano?
Heche: Niliongea
Wakili Katuga: Muda gani?
Heche: Nadhani kama nusu saa… sikumbuki
Wakili Katuga: Waambie majaji kama umeiambia mahakama siku hiyo ya mkutano uliongea
nini
Heche: Sikumbuki
Wakili Katuga: Ulimsikia mwenyekiti akisema tutazuia uchaguzi?
Heche: Ndiyo
Wakili Katuga: Ulisikia mwenyekiti akisema tutauvuruga uchaguzi?
Heche: Nilisikia.
Wakili Katuga: Waambie majaji kama mwenyekiti alisema tutahamasisha uasi
Heche: Sijasikia
Wakili Katuga: Ulisikia kama mwenyekiti alisema majaji ni ma ccm
Heche: Nilisikia
Wakili Katuga: Waambie kama alisema mahakamani hakuendeki?
Heche: Alisema
Wakili Katuga: Waambie waheshimiwa Majaji kama mwenyekiti alisema mwenyekiti alisema
mapolisi wanaingiza kura feki
Heche: Alisema
Wakili Katuga: Unajua au hujui kwamba pamoja na kesi hii, Tumdu lissu anashtakiwa kwa
kutoa taarifa za uongo mtandanoni?
Heche: Sijui
Wakili Katuga: Waambie majaji unajua au hujui kwamba mshtakiwa kwenye kesi ya kisutu
hoja ya awali alisema majaji ni ma CCM?
Heche: Sijui
Wakili Katuga: Unajua au hujui, ushahidi wako huu uliotoa hapa unaweza kutumika kwenye
hiyo kesi.
Heche: Sijui
Wakili Katuga: waambie majaji kama mwenyekiti aliwaambia au hakuwaambia njia za
kuchukua kuvuruga uchaguzi
Heche: Yes, hakutuambia
Wakili Katuga: Waambie mamaji kama lissu aliwaambia au hakuwaambia njia za kuzuia
uchaguzi
Heche: Hakutuambia
Wakili Katuga: Sema kama aliwaambia au aliwaambia njia za kuhamasisha uasi
Heche: Hakutuambia.
Wakili Katuga: Njia ya kukinukisha je
Heche: Hakusema
Wakili Katuga: Katika ushahidi wako, waambie majaji kama ulisema kama mwenyekiti
alisema muhamasishe uasi dhidi ya nani?
Heche: Nilieleza
Wakili Katuga: ni ushahidi wako kwamba uasibilikuwa uanzishwe dhidi ya tume ya
uchaguzi?
Heche: Nikweli.
#############
Wakili Katuga: Ni kweli au si kweli wewe na Lissu mlichaguliwa kwenye mkutano mkuu
Heche: Ni kweli
Wakili Katuga: Ni kweli Polisi walihusika na ulinzi
Heche: Sijui
nilikuwa ndani.
Wakili Katuga: Waambie majaji kama polisi walihusika kuingizabkura ili wewe ushinde
Heche: Sijui hilo
Wakili Katuga: Nani anahusika na kutangaza tarehe za uchaguzi mkuu kwa mujibu wa sheria za Tanzania
Heche: Sijui
Wakili Katuga: Kikatiba unajua au huji tume ya taifa ya uchaguzi inaelekeza tume kutoingiliwa na mtu
yoyote wakati wa kutekeleza majukumu yake?
Heche: Tume ipi.
Kuna kume ya uchaguzi na tume hiru ya uchaguzi na vitu viwili tofauti.
Wakili Katuga: Unajua au hujui?
Heche: Najua
Wakili Katuga: Waambie majaji kama hayo yamesemwa kwenye ibara ya ngapi ya katiba?
Heche: Ya 74
Wakili Katuga: Unajua au hujui kwamba chadema kwa mujibubwa katiba yake kinaamini demokrasia ya vyama
vingi?
Heche: Sahihi
Wakili Katuga: Unajua au hujui kwamba no reforms no election ni msimamo wa chama cha Chadema
Heche: Sahihi
Wakili Katuga: Kama makamu mwenyekiti unajua au hujui kikatiba chadema ina haki ya kuamua kudhiriki au
kutoshiriki uchaguzi Mkuu
Heche: Hilo liko wazi
Wakili Katuga: Unajua kuna vyama vingapi vya siasa vilivyosajiliwa?
Heche: Vingine ni majina tu
Wakili Katuga: Kuna vyama vingapi vilivyosajiliwa?
Heche: 19
Wakili Katuga: Unajua au hujui hivi vyama vingine ukitoa chadema, vina misimamo yao kuhusiana na
Uchaguzi?
Heche: Sijui
Wakili Katuga: Unajua au hujui uchaguzi mkuu upo kwa mujibu wa katiba
Heche: Uchaguzi huru na haki upo kwa mujibu wa katiba. Najua
Wakili Katuga: Waambie majaji kama ni haki kikatiba kwa vyama vingine kushiriki uchaguzi?
Heche: Huru na haki, ni haki washiriki usio Huru na haki siyo haki washiriki
Wakili Katuga: Waambie waheshimiwa kwenye katiba hiyo ni wapi waliyoandika hayo
uliyosema
Heche: Ibara ya 27 (2) inaruhusu kupiga vita matumizi mabaya ya mali za umma.
Wakili Katuga: Waambie waheshimiwa Majaji, kwa vile ulivyosoma hati ya mashtaka, unajua mshtakiwa anashtakiwa na aina gani ya
uhaini?
Heche: kuitishia serikali
Wakili Katuga: Wambie majaji kama unajua au hujui kwamba mshtakiwa ameshtakiwa kwa
kuchapisha na kutoa maneno kwa nia ya kuitishia serikali?
Heche: Nafahamu
Wakili Katuga: Waambie majaji, hapo kuna kosa la kuitishia serikali au nia ya kuitishia serikali?
Heche: Nia
Wakili Katuga: Swala la serikali kutishika au kutotishika ni kiini cha shtaka au siyo kiini cha shtaka?
Heche: Sijui mimi
Wakili Katuga: Kwenye ile video uliyosema kwambali ni wewe ila siyo wewe unakumbuka ulisema nini
Heche: Nakumbuka
unaweza kuwa klumeiokota huko mtandaoni, kuna mambo mengi
##############
Wakili Katuga: Ni kweli au si kweli, baada ya mshtakiwa kukamatwa kwa kesi hii, wewe uliendeleza nia ya
kuzuia uchaguzi mkuu, ni kweli au siyo kweli?
Heche: Niliendeleza
msimamo wa no Reforms No Election
Wakili Katuga: Ni kweli au si kweli wewe uliendeleza nia ya kuzuia uchaguzi
Heche: Hicho unachouliza
siyo kweli
Wakili Katuga: Unakumbuka au hukumbuki kupitia vyombo vya habari uliwahi kutangaza
uchaguzi wa 2025 hautofanyika?
Heche: Sikumbuki
Wakili Katuga: Unakumbuka au hukumbuki kwamba ulieleza katika kuzuia uchaguzi mlionana na watu mbali
mbali wa dini?
Heche: Sikumbuki
Wakili Katuga: Sema kama ulieleza kwamba mliwatembelea viongozi wa dini
Heche: Nilieleza
Wakili Katuga: Waeleze majaji kama kuna ufanano je ushshidi wa kuwatembelea viongozi wa dini na huu
uliotoa hapa mahakamani unafanana au haufanani
Heche: Mimi
sikumbuki
Wakili Katuga: Unakumbuka au hukumbuki, uliutangazia umma wa watanzania kupitia earadio kwamba siyo tu
chadema hawatashiriki bali uchaguzi hautafanyika.
Heche: Nilishaenda
pale maranyingi, sikumbuki.
Wakili Katuga: Upo tayari
kukumbushwa
Heche: Sipo tayari
(Wakili katuga akaomba mahakama amkumbushe heche kwa ushahidi huo wa sauti akiwa East
Africa Radio (Earadio))
Lissu
akasimama na kutaka Wakili wa serikali asiruhusiwe kufanya anachotaka kufanya
yaani kuthibitisha maneno yake kwa njia ya sauti. Huku Lissu akirejea kifungu
husika cha 177 (1) na 2 cha sheria ya ushahidi) akisema jambo hilo
haliwezekani.(majaji wakasema kwamba Akumbushwe na asikilizishwe sauti hiyo)
Wakili Katuga: waambie majaji hiyo nyara, hicho ukichosikia, je kina ushahidi wowote
unaofanana na ushshidi ukiotoa in chief (ushahidi wa msingi)?
Heche: sahihi
Wakili Katuga: Ni kweli hiyo nyaraka inastahili wa kwamba mtaonana na watu waliowahi kuwa
viongozi?
Heche: ni sahihi
Wakili Katuga: ni sahihi jana ulisema mlionana na Mzee Warioba?
Heche: nilisema
Wakili Katuga: Ni kweli au sio kweli kwamba uliwahi kuzungumza na EAradio
Heche: Sikumbuki
Wakili Katuga: pamoja na kukumbushwa bado hukumbuki?
Heche: Sijui
sikumbuki.
Wakili Katuga: waambie majaji ni wewe ulieleza kwamba ulisikiliz hotuba ya jaji chande
yote.
Heche: nilieleza jana
Wakili Katuga: ulieleza kwamba fijo za Oktoba 29 zililenga kuzuia uchaguzi?
Heche: eneo
hilo sikumbuki.
Wakili Katuga: unakumbuka au hukumbuki kwamba hotuba ya jaji chande ilisema fijo zile
zilisababisha na viongozi wa vyama vya siasa waliokuwa na madai mengi ya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi?
Heche: sikumbuki
Wakili Katuga: unakumbuka ulisema jaji chande alisema askari 16 waliuawa
Heche: sina
kumbukumbu hiyo
Wakili Katuga: unakumbuka jaji chande kama anasema matukio yale yalipangwa na
kuratibiwa?
Heche: hiyo
nakumbuka.
Wakili Katuga: waambie majaji kama unakumbuka ulisema mpo determined kupitia ushshidi
uliopewa?
Heche: maneno hayo yapo
Wakili Katuga: ulisema hakuna makosa ya kuzuia uchaguzi?
Heche: nilisema
Wakili Katuga: kwa uelewa wako mdogo wa sheria, ni sheria ipi inasema hayakuwa makosa
kuokoa uchaguzi
Heche: kwa
ufahamu wangu
Wakili Katuga: Waambie majaji kama moja ya malalamiko yenu, kwamba tume ya uchaguzi
ndiyo ina mamlaka ya kupanga majimbo.
Heche: tume
huru siyo hiyo unayoitaja wewe
Wakili Katuga: waambie majaji, unajua au hujui ni nani anayepanga majimbo ya uchaguzi?
Heche: ni
waziri
Wakili Katuga: Kwa ridhaa ya makama hii tukufu tusomee ibara ya 75 (3) ya Katiba.
Heche: (Akasoma ibara hiyo ambayo Inahusiana na ugawaji wa majimbo ya uchaguzi)
Wakili Katuga: wasomee hiyohiyo 75 (4)
Heche: (akasoma tena)
Wakili Katuga: ni kweli kwamba kwa mujibu wa ulichosoma tume inaangalia idadi ya watu
ikitaka kugawa jimbo?
Heche: ibara
ya 74
Wakili Katuga: tuambie, ni wewe au siyo wewe uliyeiambia mahakama tukufu kwamba hotuba
ya mwenyekiti hakutoa njia ya kuzuia uchaguzi
Heche: sijui
Wakili Katuga: ni haki au si haki kwa aliyehamasika na hotuba hiyo kutumia njia yoyote
kuuvurga uchaguzi?
Heche: sijui
Wakili Katuga: ni haki kwa yoyote kufanya lolote ili kuweza kukinukisha?
Heche: sijui
Wakili Katuga: waambie majaji kama kuchoma vituo vya kupigia kura ni njia mojawapo ya
kuzuia uchaguzi au siyo njia moja wapo?
Heche: Sijui
Wakili Katuga: waambie majaji, kama kuanzisha fujo, kuchoma vituo, majengo,
mwendokasi, mafuta kunaweza kuvunja amani?
Heche: sijui
Wakili Katuga: waambie majaji kama kuna fujo ambayo haiwezekani kuwa contained inaweza au
haiwezi kuzuia kupiga kura?
Heche: Sijui.
Wakili Katuga: waambie majaji kama kukata watu vidole waliopiga kura, kunaweza kuwatisha watu wengine wasiende
kupiga kura
Heche: sijui
Wakili Katuga: waambie waheshimiwa Majaji, kama katika ushahidi wako, ulieleza hapa mahakamani kwamba hii nia ya kuzuia
uchaguzi tulikuwa tunafanya hivi…
Heche: nilieleza vizuri sana
Wakili Katuga: Kwamba mipango kufanya uchaguzi kwa kumtembelea jaji Warioba?
Heche: Si
sahihi
Wakili Katuga: mlipanga kuzuia uchaguzi kwa kumtembelea sheikh ponda?
Heche: Ni
sahihi.
Wakili Katuga: ni kweli au si kweli, kuchoma vituo vya kupigia kura ni uasi djidi ya
tume ya uchaguzi?
Heche: siyo
kweli
Wakili Katuga: tupe tafsiri ya uasi
Heche: kukataa mfumo mbovu, kukataa wazi wa kura
Wakili Katuga: vituo vya kupigia kura vinasimamiwa na nani?
Heche: Sijui.
Wakili Katuga: Vinasimamiwa na nani
Heche: Na
tume
Wakili Katuga: ukichoma kituo cha kupigia kura, unakuwa umefanya kosa dhidi ya nani?
Heche: Dhidi
ya tume.
Wakili Katuga: Ulisema kwenye ushahidi wa msingi kwamba tume ya chande haikuwahi
kukuota hata kidogo?
Heche: Nilisema
jana
Wakili Katuga: Ulisema tume hiyo haijawahi kabisa kuita chama chenu?
Heche: Sikusema hivyo, nilisema sina kumbukumbu ya kuitwa kwa chama chetu
Wakili Katuga: unajua au hujui kama moja ya njia ya serikali kutangaza taarifa ni
kupitia gazeti la aserikali
Heche: Sijui.
Wakili Katuga: Unajua au hujui kama tume ya jaji chande ilisema kwenye gazeti la serikali
kwamba kuna watu wanawazuia wengine kwenda kutoa maoni kwenye tume hiyo?
Heche: Sijui.
Wakili Katuga: unajua au hujui kama uliitwa na tume ya jaji chande ukafafanue baadhi ya
kauli zako?
Heche: sikuwahi kuitwa?
Wakili Katuga: Waambie majaji kama unajua au hujui kama tume ilitangaza kupitia
platforms mbalimbali kwa watanzania wote kwenda kutoa maoni kuhusu matukio ya Oktoba
29.
Heche: Sijui.
Wakili Katuga: Na wewe unasema unaishi wapi? Tanzania au Kenya?
Heche: Sijui
Wakili Katuga: Unakumbuka uliwahi kuitwa na tume?
Heche: Sikuwahi
kuitwa
Wakili Katuga: nikuletee uthibitisho wa kuitwa kwako?
Wakili Katuga anampa heche nyaraka ambayo ni barua inayo mtaja John Heche kama makamu
mwenyekiti wa CHADEMA.
Heche anaitazama
na kuisoma
Wakili Katuga: Waambie majaji kama sanduku la posta 31191 ni la chadema?
Heche: Ni la
Chadema.
Wakili Katuga: Wambie majaji inaonesha tarehe ngapi?
Heche: Tarehe
22, 2025
Wakili Katuga: Waambie majaji hiyo barua imeshindwa na nani.
Heche: Imesainiwa na Nijole
Wakili Katuga: Ni kweli au si kweli barua hii ilikuwa ni kutaka kuwasilisha taarifa kwa tume
Heche: Ni
sahihi.
Wakili Katuga: Kwa ridhaa ya mahakama nikuonyeshe barua ya pili, ni kutoka wapi?
(Wakili katuga akampa heche barua ya pili).
Heche anaipokea.
Wakili Katuga: Waambie waheshimiwa inatoka wapi?
Heche: Inatoka
kwenye tume.
Wakili Katuga: Ni barua ya tarehe ngapi?
Heche: 21
Wakili Katuga: waambie majaji hiyo barua ilikuwa na kichwa gani cha habari?
Heche: akasoma kikiwa kinahusiana na wito wa kwenda yah wito wa kukutana na tume ya
rais kuzungumzia matukio ya Oktoba 2025.
Wakili Katuga: Na hiyo imesainiwa na nani?
Heche: Imesainiwa
na Honorus Njohole.
Wakili Katuga: Wakili katuga akaomba mahakama ampatie heche barua nyingine inayohusu
wito
Heche: akipokea na kuisoma
Wakili Katuga: kichwa cha habari kilihusiana na nini?
Heche: Kuitwa na tume ya rais kuhusu matukio ta oktoba 29, 2025.
Wakili Katuga: Hiyo ilikuwa kwa nani?
Heche: ilielekezwa kwa
kwa katibu mkuu
Wakili Katuga: Je ungependa barua hizi zipokelewe hapa mahakamani kama ushahidi?
Heche: Hapana, Sitaki.
Wakili Katuga: Kwa ridhaa ya mahakama, unajua au hujui kama tume ilitoa tangazo kwa
umma kwamba ipo tayari kupokea maandishi, nyaraka, picha na vingine kwamba
kwa asiyetaka kwenda atume hivyo vielelezo?
Heche: Sijui
Wakili Katuga anampa Heche nyaraka mwingine ambayo inahusiana na taarifa ya tume
kuhusu kubalika umma na wadau wote kwenda kutoa ushahidi wa matukio ya Oktoba
29 ikiwemo kutuma kwa njia za sms na WhatsApp na barua pepe kwa ambaye hatakuwa
tayari kwenda mbele ya tume hiyo).
Heche: Heche
akapokea na kuisoma.
Wakili Katuga: Wewe ni sehemu ya Watanzania au siyo?
Heche: Mimi
ni sehemu ya Watanzania.
Wakili Katuga akaomba mahakama ampe Lissu Nyaraka Nyingine ilia kumwonesha kama sehemu ya
ushshisi, alimpa nyaraka ambayo ilikuwa ni taarifa kwa umma iliyotolewa na tume
ya uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29, 2025 ambayo heche aliisoma ikonesha
Heche:
Wakili Katuga: Unakumbuka au hukimbuki ulisema
tume ya jaji chande hamkuikubali kama chadema wala kuipa ushirikiano?
Heche: Nilisema hatukubali muundo wake
Wakili Katuga: Kutowapa ushirikiano?
Heche: Sikusema
hilo
