
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan leo, tarehe 16 Novemba, 2026, amekutana na kufanya majadiliano na wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Rais amelishukuru Baraza pamoja na viongozi wa vyama vya siasa kwa utayari wao wa siku zote kufanya mazungumzo na majadiliano ya kuimarisha misingi ya Taifa letu.
“Sasa ni wakati mwingine wa kuendeleza mashauriano na wadau wa kisiasa, taasisi za kiraia na sekta binafsi kwa kuunda Tume ya Maridhiano na Upatanishi, itakayoratibu maandalizi ya mchakato wa Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”
Kwa upande wao, pamoja na mambo mengine, wajumbe wa Baraza wamependekeza Tume ya Maridhiano itakayoundwa iwe jumuishi kwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili za Muungano na usawa wa kijinsia.
Kikao cha Rais Dkt. Samia na Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa kinaendeleza hatua za mashauriano ya Rais Dkt. Samia na wadau mbalimbali kuhusu mchakato wa Maridhiano. Katika nyakati tofauti, Rais Dkt. Samia alikutana na wagombea urais na wagombea wenza wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, pamoja na viongozi wa vyama vya siasa.
