
Mume wa mwanamuziki wa nyimbo za Injili Nigeria, Osinachi, Peter Nwachukwu amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya mahakama kuu ya Wilaya ya Shirikisho Abuja, kumkuta na hatia ya kusababisha kifo cha Osinachi kwa makusudi.
Hukumu hiyo imetolewa ikiwa imepita miaka mitatu tangu Osinachi afariki dunia Aprili 8, 2022, ambapo taarifa za awali kutoka kwa mume wake zilidai Osinachi alikuwa anaugua saratani ya koo.
Hata hivyo shuhuda kutoka kwa wanafamilia na ndugu wa karibu zilibainishwa mahakamani kuwa Osinachi alikuwa akifanyiwa ukatili wa kijinsia na mume wake.
Katika moja ya Ushahidi uliotolewa mahakamani ulieleza kuwa Nwachukwu alimkanyaga Osinachi kifuani kabla ya kifo chake
Baadaye Nwachukwu alishtakiwa kwa makosa 23, yakiwemo kuua kwa makusudi, vitisho vya jinai, ukatili dhidi ya Watoto na vipigo kwa Mwenzi wa Ndoa