
Timu ya waokoaji wakiendelea na zoezi la uokoaji, jimbo la Dingri, China.
Watu 126 wamefariki dunia na wengine 188 wamejeruhiwa baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa mtikisiko 6.8 kulikumba jimbo la Dingri katika jiji la Xigaze, nchini China, Xizang. Tetemeko hilo limetoka, jana usiku saa 3:05.
Kitengo cha majanga cha Xizang, kimeeleza kuwa tetemeko hilo ni la hali ya juu, kuwahi kutokea.
Mpaka sasa watu 30,400 wamehamishiwa katika makazi ya muda, na waliojeruhiwa wanaendeela na matibabu.
Mpaka sasa watu 407 wameokolewa baada ya kunasa kwenye kifusi kilichosababishwa na tetemeko hilo.
Kihistoria, Januari 23, 1556 tetemeko linalofanana na hili lilikumba jimbo la Shaanxi nchini China na kuua takribani watu 830,000 na kuathiri makazi ya watu.